Mashabiki Al Ahly Waendelea Kumkataa Miquissone - EDUSPORTSTZ

Latest

Mashabiki Al Ahly Waendelea Kumkataa MiquissoneLicha ya Pitso Mosimane kuwapa Al Ahly taji la CAF Super Cup bado mashabiki wameendelea kumkosoa hasa baada ya Al Ahly kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Future Fc.

Mashabiki wanakosoa selection ya Kikosi kwa kuanza na Kiungo Luis Miquissone mbele ya Taher Mohamed Taher na Hussein El Shahat ambao wao wanaamini kiwango cha Luis Miquissone kinaingia zaidi ya mara milioni kwa viungo hao.

Mashabiki wanaenda mbali zaidi na kusema mpango wa kumnunua Miquissone ni uharibifu wa pesa na wana muona kama dhaifu sana.

Hata hivyo baadhi yao wamekuwa na mawazo tofauti… wengine wanamkosoa Pitso kwa kumuingiza Rami Rabia

Al Ahly wameendelea kukaa juu ya msimamo wa ligi kuu nchini Misri wakiwa na alama 19 sawa na Zamalek aliepo nafasi ya pili ila Ahly ana faida ya mchezo mmoja mkononi.

Katika mechi 7 walizocheza msimu huu,Pitso amewaongoza Al Ahly kushinda michezo 6,sare 1 na hajapoteza.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz