Wasafi Wana Ushirikiano Kama Boda Boda Msibani - EDUSPORTSTZ

Latest

Wasafi Wana Ushirikiano Kama Boda Boda Msibani


Nimefatilia kwa ukaribu sana msiba Huu wa Don Fumbwe pale mkoani Tanga. Kwa faida ya ambao bado hawana taarifa hizi ni kwamba Juzi jioni Don Fumbwe amefiwa na Baba yake mzazi na mazishi yatafanyika leo hii. Don Fumbwe ni Meneja wa RayVanny, mbali na umeneja anamichongo mingine pale wasafi.

Kiukweli msiba huu ni tofauti sana na ule msiba wa Lulu diva, msiba wa Luludiva Wasanii hawakutoa ushirikiano mzuri Sana wengi walienda kumchora tu. Huu msiba wa Don Fumbwe uko tofauti kidogo na watu wapo serious.

Kiukweli Wasafi Wanaupendo wa ajabu sana, Diamond Platnumz, Babutale, Mbosso, Wafanyakazi wa Wasafi Media, Mama Dangote , Uncle Shamte nimeona wanaingia usiku wa kuamkia leo Mkoani Tanga kwaajili ya mazishi leo hii.

Hili ni jambo kubwa sana, kiukweli wasafi wanaushirikiano mkubwa sana wanapopata matatizo au Shughuli ya Furaha.

Wale wazee wa kuchunguza kwamba Don Fumbwe kajenga au hajajenga kaeni mkao wa kula macho yahamie Wasafi Tv ili badae mpate cha kuongea.

R.I.P BABA DON FUMBWE.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz