HII NDIO TASWIRA YA YANGA SIKU MOJA KABLA YA MCHEZO WAKE NA SIMBA - EDUSPORTSTZ

Latest

HII NDIO TASWIRA YA YANGA SIKU MOJA KABLA YA MCHEZO WAKE NA SIMBANi siku moja pekee ambayo ni leo Jumamosi imesalia kuelekea mechi kubwa ya vigogo wa katika soka la Tanzania Simba na Yanga watakaokutana kwenye Uwanja wa Taifa kesho Jumapili.

Simba na Yanga zinakutana kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwa na kumbukumbu ya kwenda sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya raundi ya kwanza.

Yanga inaenda kuchuana na Simba ikiwa mgeni huku ikiwa haina uhakika wa kuwatuma baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawana hali nzuri kiafya tangu msimu huu wa 2017/18 uanze.

Wachezaji hao ni Donald Ngoma na Amis Tambwe ambao wamekosekana kwenye mechi lukuki kutokana na kuandamwa na majeruhi.

Ingawa uongozi wa Yanga umekuwa ukitangaza kuwa wachezaji hao kuwa wako fiti kila inapotokea wanakuwa na mechi, wamekuwa wakishindwa kuonekana Uwanjani sababu ya majeruhi kuwaandama.

Mbali na wawili hao, Ibrahim Ajibu, Andrew Vincent na Kelvin Yondani ndiyo waliorejea kikosini baada ya kupatwa na majeruhi siku kadhaa zilizopita.

Urejeo wa wachezaji hao unaleta manufaa kwa kikosi cha Yanga ambacho kimetawaliwa na vijana wengi kwa msimu huu baada ya wakongwe baadhi kuonekana kwa nadra Uwanjani kwa sababu tajwa hapo juu.

Credit to sarehejembe


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz