UTABIRI WA EDO KUMWEMBE KUELEKEA MECHI YA LEO KATI YA SIMBA NA YANGA - EDUSPORTSTZ

Latest

UTABIRI WA EDO KUMWEMBE KUELEKEA MECHI YA LEO KATI YA SIMBA NA YANGAMchambuzi nguli wa soka nchini Edo Kumwembe ameweka wazi kuwa timu anayoipa nafasi ya kushinda pambano la watani wa Jadi ni Simba, kutokana na aina ya wachezaji alionao msimu huu.


Akitoa utabiri wake kwenye mchezo huo leo ndani ya kipindi cha 'Shabiki On Saturday' cha East Africa TV, Edo amesema nafasi kubwa ipo kwa Simba. Ameeleza Simba imekuwa bora msimu huu ukizingatia haijapoteza mchezo hata mmoja.

''Mimi nawapa Simba 'Advantage' ya kushinda pambano la kesho kutokana na wachezaji wao watatu Okwi, Kichuya na Bocco ambao wako kwenye kiwango cha juu zaidi msimu huu hivyo wanaweza kuamua matokeo ya ushindi wa Simba,'' amesema.

Kwa upande mwingine Edo amesema pamoja na Simba kuwa na nafasi kubwa lakini wasisahau mpira unadunda. Pia ameongeza kuwa hata misimu kadhaa Yanga amewahi kuwa kwenye ubora lakini Simba walishinda kwahiyo lolote linaweza kutokea.

Timu zote mbili zilikuwa zimeweka kambi mkoani Morogoro na zinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam muda wowote jioni hii tayari kwa mchezo wa kesho ambao utaamua nani anakwenda kutwaa ubingwa.

CREDIT TO Eatv
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

WEKA EMAIL YAKO HAPA KUTUMIWA HABARI ZA MICHEZO BURE

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz