SIMBA YAWATISHA AL MASRY MAPEMAA,WAANZA KUWAVIZIA KIMYAKIMYA - EDUSPORTSTZ

Latest

SIMBA YAWATISHA AL MASRY MAPEMAA,WAANZA KUWAVIZIA KIMYAKIMYA


Image result for AL MASRY


Wakati Simba imetuma mtu mapema kwenda Djibouti kwa ajili ya maandalizi ya mechi ijayo dhidi ya Gendamarie, wanaotarajiwa kuwa wapinzani wao wameonyesha nao wako makini zaidi.


Al Masry ya Misri wanajipa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika Kombe la Shirikisho dhidi ya Buffaloes ya Zambia baada ya kushinda kwa mabao 4-0 mechi ya kwanza.


Kutokana na hivyo, wametuma mmoja wa watu wa ufundi kutoka katika benchi lao kuangalia uchezaji wa Simba, hasa inapokuwa ugenini.


“Tayari kuna mtu ameandaliwa kwenda Djibouti kuangalia mechi ya mwisho ya Simba. Hata kama itakuwa nyepesi lakini watapata uhakika namna ya mchezo wao.


“Wanafanya mambo mawili kwa wakati mmoja, hapo wanajiandaa na mechi ya pili huko Zambia. Wana asilimia themanini ya kuvuka. Hapo hapo wameanza kujiandaa na Simba,” alisema Mtanzania anayeishi nchini baada ya kuzungumza na mwandishi wetu.
Iwapo Simba itavuka, basi ina nafasi kubwa ya kukutana na Al Masry ambayo inaonekana Simba watalazimika kufanya maandalizi ya uhakika hasa.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz