CHIRWA ALIONJA JOTO LA TFF; AFUNGIWA NA KUPIGWA FAINI KALI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 15 January 2018

CHIRWA ALIONJA JOTO LA TFF; AFUNGIWA NA KUPIGWA FAINI KALI

 CHIRWAKamati ya nidhamu iliyokutana jana Jumapili, Januari 14, 2018 imepitia kesi ya mshambuliaji wa Yanga SC, Obrey Chirwa iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi iliyohusu mchezo namba 83 kati ya Yanga na Tanzania Prisons ya mbeya iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex imemfungia michezo mitatu mchezaji huyo kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Chirwa alishtakiwa kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Chirwa ambaye alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na mwakilishi wake alikiri kutenda kosa hilo.

Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia Video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna na Muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia Kanuni za Ligi Kuu kanuni ya 37 (7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2).

Chirwa amefungiwa mechi tatu na anatakiwa kulipa faina ya Tsh. 500,000 kutokana na kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Novemba 25, 2017 kwenye uwanja wa Azam Complex.

kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa na TFF, adhabu hiyo imetolewa baada Chirwa kukiri kufanya kosa hilo la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons.

Michezo mitatu ambayo Chirwa ataikosi ni Yanga vs Mwadui (Januari 17, 2018), Yanga vs Njombe Mji (Januari 21, 2018) na Yanga vs Majimaji (Januri 28, 2018) mechi zote Yanga itacheza kwenye uwanja wake wa nyumbani (Uhuru).

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
 BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ