ZIJUE ZILIZOKIKI KATIKA TETESI ZA SOKA ULAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

ZIJUE ZILIZOKIKI KATIKA TETESI ZA SOKA ULAYA


 TETESI ZA SOKA
Manchester City wamejitoa katika makubaliano ya kumsaini Sanchez na pesa zilizoitishwa na ajenti wake. (Goal)

Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20. (Guardian)

Arsenal na Chelsea wanammezea mate mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil Richarlison 20. (Sun)

Chelsea bado wako makini kumsaini mshambuliaji wa mwezi Januari kwa mkopo huku Andy Carroll wa West Ham akiwa katika nafasi nzuri wa kusainiwa. (Telegraph)

Manchester United wako tayari kumpa kipa wa miaka 27 David de Gea mkataba mpya amboa utamweka katika klabu hiyo katika taaluma yake yote.(Mirror)

Arsenal wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamleta mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29, huko Old Trafford. (Guardian)

Crystal Palace wana matumaini ya kumaliza kumsaini mshambuliaji wa Fiorentina raia wa Senegal Khouma Babacar 24 kwa pauni milioni 15. (Guardian)

Crystal Palace pia wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kipa wa Ipswich Bartosz Bialkowski. Klabu hiyo inataka zaidi ya pauni milioni 4 kwa mchezaji huyo wa miaka 30. (Sun)

Liverpool wametupilia mbali mpango wa kumsaini wing’a wa Monaco Thomas Lemarbada baada klabu hiyo kuomba pauni milioni 90 kwa mchezaji huyo wa miaka 22. (Times

Borussia Dortmund wanakaribia kutangaza kumsaini beki la Basel mswisi Manuel Akanji 22. (Ruhr Nachrichten – in German)

Meneja wa Leicester Claude Puel anasema hana hofu kwa kundoka mwezi huu kwa mAlgeria Riyad Mahrez, 26, (Leicester Mercury)

AC Milan wanasema kuwa kuwa hawawezi kumuuza kiungo wa kati mHispania Suso 24, hata kwa pauni milioni 71. (AC Milan website – in Italian)

Liverpool wapo tayari kupambana na Manchester City na Manchester United katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29. (Sunday Mirror)

Pamoja na kutaka kumsajili Sanchez, Manchester United pia wanataka kumsajili Mesut Ozil, 29. (Sunday Mirror)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuacha kumsajili Antoine Griezmann, 26, kutoka Atletico Madrid mwisho wa msimu na hata Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid, ili amsajili Sanchez na kumpa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki. (Mail on Sunday)

Manchester United wamempa Alexis Sanchez hadi siku ya Ijumaa kuamua kama anataka kwenda Old Trafford au la, vinginevyo wataachana naye. (Sunday Express)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz