TAJIRI MTATA ALIPA DORA 100 KWA AJIRI YA KUTUMIWA PESA ZAKE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 18 November 2017

TAJIRI MTATA ALIPA DORA 100 KWA AJIRI YA KUTUMIWA PESA ZAKESakata la Dk. Louis Shika, limechukua sura mpya baada ya leo, Novemba 18, 2017 kulipa kiwango cha dola 100 za Kimarekani (sawa na shilingi 220,000), kama bima ili aweze kutumiwa mabilioni yake kwa ajili ya kulipia nyumba za kifahari za Lugumi, alizoibuka mshindi kwenye mnada wake na baadaye kujikuta akiangukia kwenye mikono ya polisi kwa madai ya kuvuruga mnada.

Dk. Shika amesema malipo hayo ya kiwango hicho kwa ajili ya bima, yatawezesha kurejesha fedha zake zilizo nje ya nchi kwa sababu alikuwa akishindwa kuzipata kwa sababu ya kukosa bima kama alivyoelekezwa.

Waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye aliyeenda Shirika la Posta kuzungumza na wafanyakazi, walimkuta Dk Shika akiwa katika shirika hilo na walipozungumza naye alisema alifika hapo kwa ajili ya malipo.

Dk Shika, ambaye alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba hizo za mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Said Lugumi, alisema ametumia shirika hilo kulipa fedha hizo za bima kwa benki moja iliyoko Bangkok, Thailand.

“Kama mnavyoona hii karatasi,” alisema akionyesha fomu ya malipo.

“Nimelipa dola 100 za bima ili kukamilisha fedha zangu zije na nilipie zile nyumba. Hili la bima lilikuwa ni muhimu sana.”

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno