ZANU-PF WAMJIA JUU MGABE, WAMTAKA AJIUZULU - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 18 November 2017

ZANU-PF WAMJIA JUU MGABE, WAMTAKA AJIUZULU


Matawi ya mkoani ya chama tawala huko Zimbabwe, ZANU-PF , yameungana na kumtaka rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, ajiuzulu.

Hatua hiyo imechukuliwa huku kukiwa na taarifa za kufanyika kwa maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare, ili kuunga mkono hatua ya jeshi kuchukua udhibiti wa nchi Jumatano iliyopita.
Watu wa karibu na rais Mugabe, wakiwemo wapiganaji waandamizi walioendesha mapigano ya kudai uhuru, pamoja na makundi ya wananchi wenye msimamo wa wastani pia wamemtaka kiongozi huyo kujiuzulu.

Wakati shinikizo la kumtaka rais Mugabe ajiuzulu, kiongozi huyo jana Ijumaa (Novemba 17, 2017)alihudhuria na kushiriki katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria kilichopo Harare, ambapo alitunuku shahada mbalimbali waliohitimu katika chuo hicho, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana hadharani, tangu jeshi lilipochukua udhibiti wa nchi, na kumuweka kizuizini nyumbani kwake.

Jeshi la Zimbabwe liliamua kuchukua udhibiti wa nchi, ikiwa ni hatua ya kuingilia kati mzozo wa kisiasa unaoendelea baina ya rais Mugabe, na maafisa wa chama tawala, akiwemo makamo wa rais, Enerson Nangwaga, aliyefukuzwa na rais Mugabe wiki iliyopita. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment