OKWI AANZA KUINYATIA REKODI YA KICHUYA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 18 November 2017

OKWI AANZA KUINYATIA REKODI YA KICHUYA OKWI KUNYATIA REKODI YA KICHUYA


Mganda huyo ameanza msimu huu kwa kasi na sasa anasaka bao lake la kwanza nje ya Dar es Salaam Okwi anaitaji bao moja kuivunja rekodi ya Kichuya MSIMU uliopita katika mzunguko wa kwanza, Shiza Kichuya aliifungia Simba, mabao tisa (mechi 15), rekodi inayokaribia kuvunjwa na Emmanuel Okwi mabao nane kwa mechi tisa, akiwa mechi sita ili zifike 15.

 Kwa rekodi hiyo, Okwi yupo nyuma bao moja dhidi ya Kichuya aliyefunga mabao matano kwa msimu huu,kabla ya kupisha usajili wa dirisha dogo kama ilivyokuwa mwakajana.

 Okwi alijiunga na Simba msimu huu, ujio wake ulizua mjadala mkubwa,huku baadhi wakiamini jezi namba 25, anayoitumia Kichuya angepewa mkongwe huyo ambaye kwa sasa anatumia jezi namba saba.

 Hata hivyo Kichuya alionekana kujiandaa kisaikolojia kuhusiana na jezi namba 25 aliyokuwa anatumia Okwi zamani, pamoja na kujipanga kiuwezo ili asikae benchi kama ilivyokuwa matarajio ya wengi. Kichuya amewahi kukaririwa akisema "Naheshimu uwezo wa Okwi, kwani nimemuona akicheza na Nnimezikuta rekodi zake Simba, hilo siyo sababu ya mimi kukaa benchi, bali atageuka somo kujua amefikaje kwenye mafanikio hayo, ili na mimi nifuate nyayo zake,"alisema. Simba ndiyo ilikuwa inaongoza kwa pointi dhidi ya Yanga, kabla ya kupisha usajili wa dirisha dogo kama ilivyo kwa sasa ambapo wanaongoza kwa pointi 19 sawa na Azam, isipokuwa kwa uwiano wa mabao. 

Yanga ni Donald Ngoma ndiye alikuwa anaongoza kwa mabao sita kwa mechi 15, alizokuwa amecheza mzunguko wa kwanza, msimu uliopita, rekodi inayokaribia kuvunjwa na Ibrahim Ajibaliye na mabao matano katika mechi tisa.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno