MOURINHO AMPIGA DONGO KALI HENRIKH MKHITARYAN - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 25 November 2017

MOURINHO AMPIGA DONGO KALI HENRIKH MKHITARYAN


 DONGO LA MOURINHO KWA MKHITARYAN
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ameukosoa mchezo wa Henrikh Mkhitaryan huku Borussia Dortmund ikisema kuwa iko tayari kumsajili kwa mara nyengine mshambuliaji huyo wa Armenia

Mkhitaryan, ambaye alijiunga na United kutoka Dortmund mwezi Julai 2016 kwa dau la £26.3m, hakushirikishwa katika kikosi cha United katika mechi mbili zilizopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hatahivyo atarudi katika kikosi cha kwanza cha United katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Brighton.

Mourinho alisema kuwa kiwango cha mchezo wa Mkhitaryan kimekuwa kikipungua hatua baada ya hatua

Mkhitaryan alianzishwa mechi 10 kati ya 11 za ligi ya Uingereza kabla ya kuachwa nje baada ya kutolewa katika dakika 62 katika mechi ambayo United ilipoteza kwa Chelsea kwa 1-0 mnamo tarehe 5 mwezi Novemba.

"Sikufurahia kiwango chake cha mchezo'', alisema Mourinho kuhusu mchezaji ambaye amefunga mabao mawili pekee katika mechi 16 alizochezeshwa msimu huu.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment