RAIS JPM KUHUDHURIA UAPISHO WA UHURU KENYATTA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 25 November 2017

RAIS JPM KUHUDHURIA UAPISHO WA UHURU KENYATTA RAIS JPMRais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ni miongoni mwa viongozi mbali mbali duniani watakaohudhuria kuapishwa kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Katika taarifa iliotiwa sahihi na mkurugenzi wa idara ya habari, maelezo na msemaji mkuu wa serikali Hassan Abbas, Magufuli atajumuika na viongozi wengine katika kushuhudia kuapishwa kwa rais Kenyatta aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 mwezi Novemba.

''Serikali inautaarifu umma kuwa rais wa Jamhuri ya tanzania John Pombe magufuli ataungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuwa rais wa kipindi cha awamu ya pili'', ilisema taarifa hiyo.

Iliongezea kwamba '' Muheshimiwa Kenyatta ataapishwa siku ya Jumanne Novemba 28 2017 jijini baada ya ushindi alioupata katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo''

Maandilizi ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta siu ya jumanne yamekamilika na usalama utawekwa kwa wale watakaoshiriki kulingana na kamati ya maandalizi.

Sherehe hiyo inatarajiwa kugharimu shilingi milioni 300 za Kenya huku ikidaiwa kuwa kiwango kikubwa cha fedha hizo kitawekwa katika kuimarisha usalama.

Mwaka 2013 wakati ambapo rais Kenyatta alikuwa akiapishwa kwa mara ya kwanza, kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo ilitaka kupewa shilingi bilioni 1.2 ambazo wizara ya fedha baadaye ilizipunguza na kufikia shilingi milioni 374 huku shilingi milioni 64 zikitolewa na idara ya mahakama.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment