NAPE NNAUYE:"ACHENI KUPIGA RAMLI JUU YA KESHO YANGU" - EDUSPORTSTZ

Latest

NAPE NNAUYE:"ACHENI KUPIGA RAMLI JUU YA KESHO YANGU"


Nape Nnauye Aikana Taarifa ya Kuwa Leo Ataongea na Waandishi wa Habari

Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuweka sawa kuwa siku ya kesho Oktoba 31, 2017 hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema kuwa watu wanatunga hizo taarifa.

Nape Nnauye ametoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii na kuwataka watu waache kumzushia mambo wakiwa na lengo la kutafuta nafasi na vyeo serikalini.
"Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina 'press conference' kesho" aliandika Nape Nnauye

Leo mchana watu wasio na nia nzuri na Nape Nnauye walizusha taarifa kuwa kiongozi huyo siku ya kesho Jumanne atakuwa na mkutano na waandishi wa habari jambo ambalo yeye mwenyewe amelipinga na kusema watu wanazusha taarifa hizo kwa maslahi yao wenyewe.




 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz