ALICHOPOST WEMA SEPETU KUHUSU LISSU NA NYALANDU LEO - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 31 October 2017

ALICHOPOST WEMA SEPETU KUHUSU LISSU NA NYALANDU LEO


Kauli ya Wema Sepetu Kuhusu Hali ya Tundu Lissu na Nyalandu Kuihama CCM

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa anajisikia furaha na amani kuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa anaendelea vyema kadili siku zinavyokwenda lakini pia amegusia sakata la Nyalandu kujitoa CCM.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa anakula chakula akiwa hospitali Nairobi na kusema anajisikia vizuri kuona shujaa wao anaendelea vizuri.

"Ni jambo jema kumuona shujaa wetu anaendelea vyema kweli Mungu ni mwema siku zote, lakini pia nikiwa mkubwa nitahitaji kuwa kama Lazaro Nyalandu" aliandika Wema Sepetu

Wema Sepetu ameweka ujumbe huu masaa kadhaa toka Lazaro Nyalandu alipotangaza kujivua uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuandika barua kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kuomba kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment