MORATA:NIPO TAYARI KUISHI LONDON KWA MIAKA 10 - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 31 October 2017

MORATA:NIPO TAYARI KUISHI LONDON KWA MIAKA 10


Morata amewahi kukiri kusikitishwa na kitendo cha kuzomewa na mashabiki wa Chelsea

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata amekanusha uvumi kwamba hapendi kuishi jiji la London na yupo tiyari kusaini mkataba wa miaka kumi kama itawezekana.

Awali Morata aliliambia gazeti moja la Italia kwamba hana maisha marefu katika jiji la London.

Alipoulizwa kuhusiana na kauli hiyo wakati akijiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Jumanne dhidi ya Roma, alisema alimaanisha hatokaa London baada ya kustaafu soka.

''Nina furaha sana hapa, na ninafurahia kila kitu cha London mimi na mke wangu,''alisema.

Morata mwenye miaka 25 amefunga magoli saba katika michezo 13 tokea aliposajiliwa kwa Pauni Milioni 60 kutoka klabu ya Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment