Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikael Mbowe, amemkaribisha
aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM , Lazaro Nyalandu baada ya kuweka wazi matamanio yake wapi pa kwenda baada ya kujiuzulu.
Mwenyekiti Mbowe ametoa fursa ya kumkaribisha ndani ya chama hicho Mhe. Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumwambia kuwa hata masuala aliyoyaibua yalikuwa ni ajenda ya chama chao kwa muda mrefu.
"Milango iko wazi kwako Lazaro Nyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu"ameandika Mh. Mbowe.
Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM jana alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.
Follow
Freeman Mbowe
✔@freemanmbowetz
Milango iko wazi kwako @LazaroNyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu.
7:36 PM - Oct 30, 2017
112112 Replies
151151 Retweets
999999 likes
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment