USILOLIJUA KUHUSU MTO RUAHA MKUU - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Sunday, 13 August 2017

USILOLIJUA KUHUSU MTO RUAHA MKUUMTO Ruaha Mkuu ni mto wa pili kwa kwa Urefu nchini Tanzania ambao una urefu wa km 475
, muonekano na uzuri wa mto huo huonekana vizuri sana katika uwanda wa Bonde la Usangu na katika hifadhi ya Taifa ya RuahaAsili ya jina la Ruaha mkuu ninatokana na Lugha ya Kihehe yani RUVAHA yenye maana mto mkubwa na mto huo kwa wenyeji wa bonge la Usangu (Wasangu) hufahamika kwajina la (MNYINAVANA) kwa maana ya mto mkubwa ni moja ya mito yenye kona na mzunguko wa wajabu sana na pia humwaga maji kwa kiwango kikubwa katika eneo chepechepe la Ihefu (Ihefu Swamp) kabla ya kuunganika na kuendelea.

Ukubwa wa mto Ruaha Mkuu ni Km za Mraba 83,970 na muda mrefu mto huo umekuwa ukitumika kwajili ya shughuri za kilimo cha umwagiliaji,uvuvi na kunyweshea mifugo, matumizi ya wanyama wa porini katika eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha na pia mto huo umekuwa ukitumika kama chanzo cha umeme katika mabwawa ya Mtera na Kidatu.

Chanzo cha Mto Ruaha mkuu ni safu za Milima ya Kipengere na huunganika na mito mbalimbali ikiwemo ya Lukosi, Yovi, Kitete, Sanje,Kimbi,Nyamalela, Ruaha-mdogo, Kisigo, Mbarali(Barali),Kimani na Chimala pamoja na mito modogo ya Umrobo, Mkoji, Lunwa, Mlomboji, Ipatagwa, Mambi na Mswiswi na kuambaa katika uwanda wa bonde la Usangu wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.

Maajabu ya mto Ruaha Mkuu ni kuwa una aina 38 za samaki wakiwemo Kitoga,kolokolo na kambale na pia ni mazalia ya wanyama wakiwemo viboko, Mamba na kenge wakubwa,hata hivyo mto huo umekuwa ukiathiliwa na shughuri za kibinadamu na mwanzoni mwa miaka ya 1990 hadi mwaka 1994 mto huo ulianza kukauka nyakati za kiangazi na kubakiza madibwi tu ingawa kumekuwa na jitihada za makusudi za kuhifadhi asili ya mto huo.


Na mto wa kwanza kwa urefu nchini Tanzania ni Mto Rufiji ambao ambao unakadiliwa kuwa na urefu wa Km 600 na chanzo cha mto huo ni mito ya kilombero na Luwegu na umekuwa ukimwaga maji katika bahari ya hindi katika mkondo wa eneo la Kisiwa cha mafia.