USAIN BOLT AUMIA AKIWA MBIONI - EDUSPORTSTZ

Latest

USAIN BOLT AUMIA AKIWA MBIONI

Usain Bolt akiwa chini baada ya kuumia na kushindwa kumaliza mbio zake za mwisho za ubingwa wa dunia jijini London.
…Akiwa chini baada ya kuanguka na kuumia.
…Akiwa ameshikwa na msuli.

Usain Bolt jana aliumia na kushindwa kumaliza mbio zake za mwisho za ubingwa wa dunia jijini London, na mwanariadha mwenzake Yohan Blake anasema huenda kucheleweshwa kwa mbio hizo kulimwathiri.

Bolt alipata mkakamao wa misuli na kulazimika kuondoka uwanjani alipokuwa akikimbia mbio za kupokezana vijiti za 4x100m ambazo timu ya Uingereza ilishinda.

Yohan Blake alisema: “Mbio zilicheleweshwa dakika 10, tuliwekwa tukisubiri kwa dakika 40. Ilitushangaza sana.”

Bolt alikuwa ametumaini angemaliza maisha yake ya ukimbiaji kwa kushinda dhahabu mbili mashindano hayo ya London lakini ameondoka na nishani ya shaba pekee aliyoshinda kwenye mbio za mita 100 wikendi iliyopita.

Sekunde chache baada yake kupokezwa kijiti awamu ya mwisho ya mbio hizo, alishikwa msuli na kuanguka.

Daktari wa timu ya Jamaica Kevin Jones amethibitisha kwamba Bolt alipatwa na mkakamao wa misuli ya mguu wake wa kushoto.

“Tulikaa tukipasha misuli na kusubiri, kisha tunapasha misuli tena na kusubiri. Nadhani hilo lilituathiri,” alisema Blake.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz