SEMINA KALI KUTOLEWA KWA WANAFUNZI: MIMI NI MSHINDI NAJIKUBALI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Friday, 11 August 2017

SEMINA KALI KUTOLEWA KWA WANAFUNZI: MIMI NI MSHINDI NAJIKUBALI
WANAFUNZI WA MAGAMBA SEC WAKATI WAKIJIBU MASWALI

Leo tarehe 11 mwezi wa 8 imetolewa semina kwa wanafunzi wa shule ya magamba iliyoko kata ya  Magamba ,Lushoto Tanga. Semina hiyo imetolewa na timu ya vijina wenye ushawishi katika kuhamasisha maswala mbali mbali ya kimaisha.

MADA KUU. Mada kuu ilipewa jina lenye ushawishi na kuvutia kwa kila aliyelisikia ikiwa ni
                                          MIMI NI MSHINDI NAJIKUBALI.
MKUU WA SHULE NDG PETER NYELLO AKIFANYA UTAMBULISHO


MR LUI MUSH; “We ni mshindi , jiamini na jikubali kuwa wewe ni wapekee hufanani na mtu yeyote"MR BONNY “ Adui uliyenaye katika safari yako ya maishi ni ofu (WOGA),kuwajasiri wewe ni mshindi”


BAKALEMWA TZ “ Ndoto ndiyo maisha yako halisi uliyo umbiwa, ishi katika ndoto wewe ni shujaa”

MADA NDOGONDOGO:

1. Thamani ya kujiami by LUI MUSHI #mind advisory

2. Mambo yanayokufanya usifanikiwe by MR BONNY

3. Jinsi ya kuishi ndoto zako by BAKALEMWA TZ #MindCourchTrainer

WALENGWA: Semina hii imetolewa mahususi kwa wanafunzi wote ilikujenga fikira chanya juu ya kufanya ndoto zao zitimie.

LENGO: kusudi na nia ya dhati ilikua ni, kutoa hamasa, kuamsha na kuzitia faraja moyo ya wanafunzi kupitia kauli mbiu mimi ni mshindi najikubali. NB;semina hii itaendele kutulewa kwa shule nyinginezo mkoani na Tanzania kote.

MADHUMUNI: Wahamasishaji hawa wamekusudia kutumia karama yao ya pekee katika mambo yafuatayo;

· Kujenga mtazamo chanya baina ya wanafuzi

· Kuandaa taifa la watu jasiri na wenye kufikiri mambo makubwa yenye uwezo wakutatua changamoto za kimaisha

· Kurejesha faraja kwa waliopoteza matumaini

· Kuonesha njia sahihi ya kufikia malengo yasiyo na mipaka

· Kuwakuza watu kifikira juu ya uwezo wa ziada walio nao katika kufikia ndoto zao.


SHUKURANI: Wahamasishaji hao chini ya kivuri cha ODAF (One direction art forum) wanatoa pongezi kwa Mkuu wa shule hiyo Mwl Peter Nyello pamoja na uongozi wa shule hiyo kwa mapokezi na ukarimu wao.

MAWASILIANO: Waweza kuwasiliana na wahamasishaji hawa kwa shughuri yeyote ya kiushauri au semina kwa mawasiliano ya fuatayo:

A. BakalemwaTz call +2557441463

B. Lui Mushi call +255766988026

C. Mr Bonny call +25514106228

IKUMBUKWE NAMBA HIZI NI KWA AJILI YA SEMINA NA USHAURI TU