Yanga wataenda zenji kujipanga upya - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga wataenda zenji kujipanga upya




Kikosi cha Yanga kimepanga kwenda kuweka kambi ya pamoja Pemba, Zanzibar kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii watakayocheza dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kambi hiyo itakuwa ya pili kwa Yanga kutoka nje ya Jiji la Dar es Salaam baada ya hivi karibuni kurejea kutokea Bigwa mkoani Morogoro ambako walikaa kwa wiki mbili.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema wameichagua Pemba kutokana na utulivu ili Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina apate nafasi ya kukiandaa kikosi hicho vizuri.

Mkwasa alisema, timu hiyo itarejea jijini Dar siku moja kabla ya mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.

Aliongeza kuwa, maandalizi ya kambi hiyo tayari yamekamilika na wametuma watu kwa ajili ya kuandaa kambi hiyo itakayofikia timu yao.

"Tutaondoka Dar Jumapili asubuhi kuelekea Unguja, hapo tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege, usiku wa siku hiyohiyo, baada ya hapo Jumatatu tutaondoka kwenda Pemba," alisema Mkwasa.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz