Jioni ya leo mabingwa watetezi wa kombe la CRDB Yanga watashuka uwanja wa CC Kirumba kumenyana na Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.
Ni Dar es salaam Derby inapigwa kwenye uwanja w CCM Kirumba jijini Mwanza ikizikutanisha timu mbili zenye ushindani wa aina yake.
Hii itakuwa mara ya tatu timu hizi zinakutana msimu huu, Yanga ikishinda mechi ya kombe la Muungano huku mechi ya kwanza ya ligi ikimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Leo lazima mshindi apatikane hivyo kama dakika 90 zitamalizika kwa sare, kutakuwa na dakika 30 za nyongeza na mikwaju ya penati.
Yanga itaingia katika mchezo huo ikisaka ushindi katika msimu wa sita mfululizo wakicheza nusu fainali. Yanga haijapoteza mchezo wa kombe la Shirikisho (FA) kwa takribani miaka mitano wakishinda mechi 28 mfululizo.
Katika kipindi chote cha utawala wao kwenye michuano hiyo, hawajapoteza mchezo dhidi ya Azam Fc na hivyo kufanya mchezo wa leo kuwa mgumu zaidi.
Kwa upande wa Azam Fc, matumaini yao ya kutwaa taji msimu huu yamesalia kwenye kombe la CRDB hivyo mechi ya leo wanaichukulia kwa uzito mkubwa.
Kocha wa timu hiyo Florent Ibenge ameweka wazi kuwa leo wanataka kuwapa furaha mashabiki wao ambao kila mara walipokutana na Yanga katika michuano hiyo wametoka vichwa chini.
Hata hivyo bado haitakuwa rahisi kwao kwani Yanga imejipambanua kuwa timu ngumu kufungika zinapofika hatua hizi za mwishoni.
Wananchi ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa misimu minne mfululizo na msimu huu wanalisaka taji la tano.
Baada ya Simba kuifunga Coastal Union jana na kutangulia fainali, ni wazi Yanga inakwenda kupambana kusaka ushindi ili wakutane na watani zao katika mchezo wa fainali.
Usikose kuitazama live kupitia simu yako kupitia app yetu
Bonyeza hapa kudownload App hii utazame sasa
Usikose kutazama mechi zote LIVE kupitia simu yako pia ukiwa na App hii utaweza kutazama mechi zA Caf, mechi zote za ulaya, ligi kuu Tanzania bara, CRDB CUP na nyingine nyingi LIVE kupitia Simu yako
download App hii mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA AU HAPAAAA au HAPAA

Post a Comment