BAADA ya kusubiri kwa miaka 22, Arsenal imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) kwa aina yake kufuatia mpinzani wake mkubwa, Manchester City kutoka sare ya 1-1 dhidi ya AFC Bournemouth katika mechi inayotarajiwa kuwa ya pili kutoka mwisho kwa kocha Pep Guardiola akiwa benchi la City.
Matokeo hayo ya usiku wa Jumanne ya Mei 19, 2026, yaliyopatikana kwenye Uwanja wa Bournemouth, yanaiacha Arsenal FC ikiwa mbele kwa pointi nne dhidi ya City kabla ya michezo ya mwisho ya msimu kupigwa Jumapili ijayo, huku kikosi cha Mikel Arteta kikitarajiwa kukabidhiwa kombe baada ya mechi na Crystal Palace.
Maandalizi ya mchezo huo yalitawaliwa na taarifa zilizozua taharuki zikidai kuwa Guardiola anatarajia kuondoka City mwishoni mwa msimu huu.
Guardiola aliwaambia watangazaji wa televisheni kabla ya mechi kuwa uvumi kuhusu mustakabali wake haukuwa na athari yoyote kabisa kwenye maandalizi ya kikosi chake, lakini City ilizidiwa uwezo na nguvu na Bournemouth iliyokuwa bora usiku huo, huku ikiongeza rekodi ya kutopoteza mechi kufikia michezo 17 mfululizo.
Ikipewa nguvu na mashabiki wake waliokuwa na shamrashamra kubwa kwenye uwanja huo wa nyumbani, kinda mshambuliaji Junior Kroupi alifunga bao maridadi dakika sita kabla ya mapumziko.
Mlinda mlango wa wenyeji, Djordje Petrovic aliokoa hatari muhimu mapema kipindi cha pili kwa kumzuia Nico O’Reilly, na licha ya Erling Haaland kusawazisha mwishoni mwa mchezo, Bournemouth ilifanikiwa kushikilia matokeo hayo na kubaki 1-1 na kukata tiketi ya kushiriki Europa League msimu ujao.
Kocha wa Bournemouth, Andoni Iraola, tayari ametangaza kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu, na matokeo haya yanamaanisha ameisaidia klabu hiyo kufanikisha mafanikio makubwa ya kufuzu kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.
The post ULIKUWA NA MIAKA MINGAPI MARA YA MWISHO ARSENAL WAKIBEBA KOMBE LA EPL? appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/0o9ax3z
via IFTTT
Post a Comment