Nilivyomfanya Mume Wangu Aache Mwanamke Aliyekuwa Akimchelewesha Kila Usiku na Kurudi Nyumbani Kabisa

Sikuwahi kufikiria kwamba siku moja ningekaa ndani ya nyumba yangu nikihisi kama nimebaki peke yangu ilhali bado nilikuwa na mume. 

Tulikuwa tumejenga maisha pamoja kwa miaka kadhaa. Tulikuwa tumepitia mengi changamoto za kifedha, kulea watoto, na vipindi vigumu vya maisha. Nilikuwa naamini hakuna kitu kingetikisa ndoa yetu kwa urahisi.

Lakini ghafla mambo yakaanza kubadilika. Mwanzoni niliona mume wangu ameanza kurudi nyumbani kuchelewa. Alikuwa anatoa sababu za kazi nyingi, meetings, au kusaidia marafiki. Nilijaribu kuelewa kwa sababu sikutaka kuwa mke wa mashaka kila wakati. Lakini kadri wiki zilivyopita, hali ilizidi kuwa mbaya.

Simu yake ilianza kuwa siri kubwa. Akipigiwa simu alikuwa anatoka nje kuzungumza. Messages zikianza kuingia usiku alikuwa anaficha simu haraka. 

Wakati mwingine alikuwa anarudi nyumbani akiwa baridi kabisa kana kwamba hataki hata mazungumzo. Kilichoniumiza zaidi ni pale nilipoanza kusikia uvumi.

Watu wa karibu walikuwa wakinidokeza kuwa alikuwa ameonekana mara kadhaa akiwa karibu sana na mwanamke mwingine. Mwanzoni sikutaka kuamini. Lakini ndani ya moyo wangu nilianza kuona kuna kitu hakikuwa sawa. Nyumbani kulianza kupoteza furaha.SOMA ZAIDI.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post