Nilivyogundua Siri ya Hasara Zilizokuwa Zikinifuata Kwenye Kila Biashara Niliyoanzisha

Kwa miaka mingi nilikuwa na ndoto kubwa za kufanikiwa kibiashara. Nilikuwa naamini ukifanya kazi kwa bidii na kuwa mvumilivu, lazima siku moja maisha yabadilike. 

Lakini kwangu mambo yalikuwa tofauti kabisa. Biashara ya kwanza niliyoanzisha ilikufa ndani ya miezi michache. Nilijiambia labda nilikosea mbinu au sikuwa na uzoefu wa kutosha.

Nikajikaza tena. Baadaye nikafungua biashara nyingine kwa matumaini makubwa. Mwanzoni ilionekana kwenda vizuri, lakini ghafla mambo yakaanza kubadilika. 

Wateja wakapungua bila sababu, bidhaa zikaanza kukwama, na mwisho nikapata hasara kubwa tena.

Nilipoanzisha biashara ya tatu, nilijaribu kuwa makini zaidi. Nilichunguza soko, nikapanga vizuri fedha, na hata nikafuata ushauri wa watu waliokuwa wamefanikiwa. 

Lakini cha kushangaza ni kwamba mambo yalirudia yale yale. Kila nilipokaribia kuona mafanikio, jambo fulani lisiloeleweka lilikuwa linatokea.

Mara bidhaa zinaharibika ghafla, mara wafanyakazi wanaondoka bila taarifa, mara madeni yanaibuka wakati ambao sikuutarajia. 

Ilifika hatua watu wa karibu wakaanza kuniambia labda biashara si kitu changu.

Kilichoniumiza zaidi ni kuona watu nilioanza nao wakifanikiwa huku mimi nikibaki pale pale.

Nilianza kupoteza confidence kabisa. Wakati mwingine nilikuwa nakaa peke yangu nikijiuliza, “Kwa nini kila kitu ninachogusa kinaishia vibaya?” Ilifika wakati nilikaribia kuacha kabisa kufanya biashara.SOMA ZAIDI.............................

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post