NI WAKATI WA KULIPIZA, MWALIMU AREJEA NA NJAA YA USHINDI

MSHAMBULIAJI wa Simba, Seleman Mwalimu amemaliza rasmi adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyokuwa amepewa na Bodi ya Ligi Tanzania, hatua inayofungua ukurasa mpya kwake kurejea uwanjani kuisaidia timu yake.

Mwalimu alikosa michezo muhimu ikiwemo dhidi ya B19, Singida na Pamba Jiji, ambapo kukosekana kwake kulionekana wazi katika safu ya ushambuliaji ya Simba iliyohitaji kasi na ubunifu wake pembeni mwa uwanja.

Katika kipindi cha adhabu hiyo, Simba  ilijitahidi kuziba pengo lake kwa kutumia wachezaji wengine wa nafasi hiyo, lakini mchango wa Mwalimu umekuwa ukitajwa kuwa wa kipekee kutokana na uwezo wake wa kupenya na kutengeneza nafasi za mabao.

Sasa baada ya kumaliza adhabu hiyo, matarajio ya mashabiki wa Simba  yameongezeka, wakiamini kurejea kwake kutaleta nguvu mpya hasa katika mbio za kusaka ushindi na kufikia malengo ya msimu.

Kurejea kwa nyota huyo kunakuja wakati muhimu ambapo ushindani wa ligi unazidi kupamba moto, kila timu ikihitaji matokeo chanya ili kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo.

Kwa upande wake, Mwalimu anatarajiwa kurejea akiwa na ari mpya na hamasa ya kuonyesha kiwango bora zaidi, akilenga kuisaidia Simba kupata matokeo chanya na kuwapa furaha mashabiki wake waliokuwa wakimkumbuka uwanjani.

The post NI WAKATI WA KULIPIZA, MWALIMU AREJEA NA NJAA YA USHINDI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/e7z0alN
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post