KAMWE AWACHAMBUA WANAOCHANGANYA USHINDANI NA

OFISA Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe, amewataka mashabiki kuacha mtazamo wa uadui kati ya timu hiyo na Simba SC, amesisitiza kuwa klabu hizo ni watani wa jadi na si maadui kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Kamwe amesema kuwa ushindani uliopo kati ya Yanga na Simba ni sehemu ya utamaduni wa soka la Tanzania, lakini haupaswi kuchukuliwa kama uadui binafsi miongoni mwa mashabiki au viongozi.

“Yanga na Simba si maadui, ni watani wa jadi. Natolea mfano baba yangu, mzee Kamwe, ni Simba na mimi ni Yanga. Je, hapo kuna uadui?” amehoji Kamwe.

Ameeleza kuwa kila inapofika siku ya Kariakoo Derby, presha na mchecheto wa mechi huongezeka kwa wachezaji na mashabiki, jambo ambalo ni la kawaida kutokana na ukubwa wa mchezo huo, hali hiyo haiashirii chuki bali ni sehemu ya ushindani wa kimichezo.

Kamwe ameongeza kuwa mara baada ya dakika 90 kukamilika, mashabiki wa pande zote mbili hurudi kuwa kitu kimoja, wakitaniana na kuendelea na maisha yao ya kawaida bila uhasama.

Akizungumzia Kariakoo Derby ijayo, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi Mosi katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, huku akitoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi na kudumisha amani pamoja na mshikamano.

The post KAMWE AWACHAMBUA WANAOCHANGANYA USHINDANI NA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/4sMd5bB
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post