YANGA YATINGA FAINALI MAPINDUZI CUP

KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 53 na kiungo mshambuliaji Max Nzengeli, aliyefunga kwa ustadi mkubwa na kuipa Yanga tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo ya heshima visiwani Zanzibar.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, timu zote zilionesha mchezo wa ushindani mkubwa huku kila upande ukitafuta bao la mapema, lakini jitihada zao ziligonga mwamba na kwenda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili Yanga walionekana kuongeza kasi na umakini zaidi, hali iliyozaa matunda baada ya Nzengeli kuifumania nyavu za Singida Black Stars, bao lililodumu hadi mwisho wa dakika 90.

Kwa ushindi huo, Yanga sasa wanajiandaa kwa mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC, ambao umepangwa kuchezwa Januari 13, 2025, katika uwanja huo huo wa New Amaan Complex, Zanzibar, wakisaka kulitwaa taji la Kombe la Mapinduzi.

The post YANGA YATINGA FAINALI MAPINDUZI CUP appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/n9Yb2zP
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post