HERSI AFUNGA DIRISHA, OKELLO ATUA JANGWANI

RAIS wa Klabu ya Yanga, Hersi Said, amefanikiwa kukamilisha dili la kumsajili kiungo mshambuliaji Allan Okello kutoka Vipers SC ya Uganda, baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya mwisho kumruhusu mchezaji huyo kuwa mali halali ya mabingwa hao wa Tanzania.

Okello anatarajiwa kutambulishwa rasmi muda wowote kuanzia sasa, huku tayari akiwa amewasili nchini na kuelekea moja kwa moja Visiwani Zanzibar kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Singida Black Stars, jambo linaloashiria ukaribu wake kuanza safari mpya ndani ya kikosi hicho cha Jangwani.

Ili kuhakikisha dili hilo linafanikiwa, Hersi alisafiri hadi nchini Uganda ambako alikutana na Rais wa Klabu ya Vipers Sports Club, Dkt. Lawrence Mulindwa, kwa ajili ya mazungumzo ya kina yaliyojikita katika masuala ya maendeleo ya soka pamoja na kuimarisha mahusiano baina ya klabu hizo mbili.

Katika kikao hicho, viongozi hao walijadiliana kwa mapana masuala ya ushirikiano wa kimkakati, huku ajenda kuu ikiwa ni hatma ya Allan Okello, ambaye baada ya majadiliano ya kina, pande zote zilifikia mwafaka wa kumruhusu mchezaji huyo kujiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili.

Kwa kukamilika kwa dili hilo, Yanga inazidi kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha kikosi kuelekea michuano ijayo ya ndani na kimataifa, huku Okello akitarajiwa kuongeza ubunifu, kasi na ufanisi katika safu ya ushambuliaji wa timu hiyo.

The post HERSI AFUNGA DIRISHA, OKELLO ATUA JANGWANI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/yCOoDJb
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post