LICHA ya Simba SC kutokuwa na mwanzo mzuri wa msimu, kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo, Clatous Chama, amesema bado hakuna sababu ya kukata tamaa amesisitiza kuwa muda upo kwa timu hiyo kuamka na kusonga mbele.
Chama amesema matokeo yasiyoridhisha waliyoyapata katika michezo ya awali hayajawavunja moyo wachezaji, kwani bado msimu una safari ndefu na nafasi ya kurekebisha makosa ipo wazi.
“Matarajio ya msimu hayajatimia kwa matokeo tuliyopata kwenye mechi za mwanzo, sio mazuri, lakini muda bado upo. Hatujachelewa, tutaamka na kufanya kazi, na mwisho wa msimu tutakuwa na furaha,” amesema Chama.
Ameeleza kuwa kilicho muhimu kwa sasa ni kuongeza nguvu, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wachezaji ili kupambana kwa ajili ya nembo ya Simba na kufanikisha malengo waliyojiwekea.
Chama amesisitiza kuwa ana imani kubwa na kikosi kilichopo, akiamini kuwa kwa bidii, nidhamu na kujituma, Simba itaweza kurejea kwenye mstari na kuonyesha kiwango kinachotarajiwa na mashabiki wake.
Akizungumzia kurejea kwake ndani ya kikosi, Chama amesema anafahamu matarajio makubwa ya mashabiki wa Simba, jambo linalompa motisha ya kuongeza juhudi, nidhamu na kujitoa kwa hali na mali ili kuisaidia timu kufikia malengo ya msimu huu.
The post SIMBA ITAAMKA NA KUSONGA MBELE, CHAMA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/RJBX6yF
via IFTTT
Post a Comment