NIKO SEHEMU YA MAFANIKIO, OKELLO

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Allan Okello, ameonesha furaha na ari kubwa mara baada ya kujiunga na klabu hiyo kongwe, amesisitiza kuwa yuko tayari kuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya timu hiyo.

Okello amesema anajivunia kuvaa jezi ya Yanga na yupo tayari kupambana kwa ajili ya heshima na malengo ya klabu.

Kupitia ujumbe mfupi aliouandika kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kutambulishwa rasmi, Okello aliweka wazi hisia zake kwa mashabiki wa Yanga.

“Nina furaha kuwa Mwananchi. Daima mbele, nyuma mwiko,” aliandika Okello, akiuambatanisha ujumbe huo na alama ya klabu pamoja na kauli mbiu maarufu ya Yanga.

Nyota huyo alitambulishwa jana usiku saa tano, hatua iliyokuja kama zawadi kwa mashabiki wa Yanga waliokuwa katika shamrashamra za kuadhimisha Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Utambulisho huo uliibua shangwe na hisia miongoni mwa Wananchi wengi waliomkaribisha kwa nderemo na matumaini mapya.

Kwa upande wa historia yake ya soka, Okello ni mchezaji wa kimataifa wa Uganda mwenye uzoefu mkubwa, aliyewahi kuzichezea klabu za KCCA FC, Paradou AC ya Algeria na Vipers SC.

Katika klabu hizo, alijijengea jina kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao pamoja na kutoa pasi za mwisho zenye macho.

Ujio wa Okello unatarajiwa kuongeza ushindani na ubunifu mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga, hasa katika safu ya ushambuliaji.

Mashabiki wa klabu hiyo sasa wanasubiri kwa hamu kumuona nyota huyo akianza kuchangia moja kwa moja mafanikio ya Yanga katika mashindano ya ndani na kimataifa.

The post NIKO SEHEMU YA MAFANIKIO, OKELLO appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/FTs2GXJ
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post