DEPU KUTUA YANGA LEO, DIRISHA DOGO

BAADA ya uongozi wa Yanga kumtambulisha rasmi kiungo Allan Okello, macho sasa yanaelekezwa kwa mshambuliaji wao mpya Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu kama Depu, ambaye anatarajiwa kutua nchini leo kuanza safari yake mpya ndani ya klabu hiyo.

Depu anatarajiwa kuwasili nchini leo tayari kwa kukamilisha taratibu zote muhimu, kabla ya kutambulishwa rasmi kama mchezaji halali wa Yanga, hatua inayoongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji wa timu hiyo.

Ujio wa mshambuliaji huyo unatarajiwa kuwapa furaha mashabiki wa Wananchi, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri kuona maboresho makubwa kwenye eneo la kufunga mabao kuelekea michezo ya ushindani inayokuja.

Kwa mujibu wa taarifa za klabu, Depu atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili, akijiunga na Emmanuel Mwanengo, Mohammed Damaro pamoja na Allan Okello ambaye alitambulishwa rasmi jana.

Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ujio wa wachezaji wapya unaongeza ushindani na ubora ndani ya kikosi, hali itakayosaidia timu kuwa imara zaidi katika mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa.

Hata hivyo, kocha huyo amebainisha kuwa anatambua wazi kuwa wachezaji wapya watahitaji muda wa kuitambua falsafa ya timu na mfumo anaoutumia, jambo linalohitaji uvumilivu na maandalizi ya kina.

“Kuna wachezaji wapya ambao wapo kwenye timu yetu na hilo ni jambo jema, lakini ninaamini watatumia muda kuitambua falsafa. Tumeanza kuwapa kile kinachostahili, na mashindano ya Kombe la Mapinduzi ni sehemu sahihi ya kuwajaribu kabla ya mashindano mengine,” amesema kocha Pedro

The post DEPU KUTUA YANGA LEO, DIRISHA DOGO appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/qag96ZC
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post