MPANZU NA AHOUA KUJIUNGA NA TIMU MUDA WOWOTE

NYOTA wawili wa kikosi cha Simba SC, Eli Mpanzu na Charles Ahoua, wanatarajiwa kujiunga na timu hiyo muda wowote kuanzia sasa, baada ya kukamilisha taratibu zao za usafiri kuelekea visiwani Zanzibar ambako kikosi kipo kambini.

Wachezaji hao hawakuwa sehemu ya msafara wa awali wa Simba uliosafiri kwenda Zanzibar, lakini uongozi wa klabu umeeleza kuwa ujio wao ni suala la muda mfupi, huku wakitarajiwa kuungana na wenzao mara watakapowasili nchini.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amethibitisha kuwa Mpanzu na Ahoua wanatarajiwa kutua nchini ndani ya siku mbili zijazo na kujiunga moja kwa moja na kikosi kinachoendelea na maandalizi yake.

Rweyemamu amesema kutokuwapo kwao kwenye safari ya awali hakuhusiani na changamoto yoyote kubwa, bali  mipango ya usafiri, mara watakapowasili wataanza mazoezi na timu bila kuchelewa.

“Tukiachilia mbali wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu za taifa, Mpanzu na Ahoua bado hawajafika lakini tunatarajia waingie ndani ya hizi siku mbili,” amesema Rweyemamu akizungumzia hali ya kikosi.

Meneja huyo ameeleza kuwa Moussa Camara pamoja na Abdulrazack Hamza hawapo kwenye kikosi kwa sasa kutokana na changamoto za majeruhi, hali inayowalazimu kuendelea na programu maalum ya matibabu na uangalizi.

Kwa kurejea kwa Mpanzu na Ahoua, Simba inatarajia kupata nguvu mpya katika kikosi chake, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuwaona nyota hao wakirejea uwanjani na kusaidia timu katika majukumu yanayoendelea.

The post MPANZU NA AHOUA KUJIUNGA NA TIMU MUDA WOWOTE appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/AMr7qta
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post