KISASI CHA KIVITA NA HESHIMA AZAM NA SIMBA

MCHEZO wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba  na Azam FC unatarajiwa kuwa wa presha kubwa, huku kila timu ikishuka dimbani ikisaka ushindi kwa sababu tofauti kisasi na heshima.

Timu hizo zitapambana kesho katika Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, zikitafuta tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo inayowakutanisha vigogo wa soka nchini na nje ya nchi.

Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu chungu ya kipigo ilichokipata dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, hali inayoongeza presha kwa wekundu hao wa Msimbazi.

Kutokana na historia hiyo, Simba inaonekana kuwa na dhamira ya kulipa kisasi na kurejesha heshima yake mbele ya Azam FC, ambao kwa sasa wanaingia mchezo huo wakiwa na morali ya ushindi wa awali dhidi ya wapinzani wao hao.

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker amesema kikosi chake kimefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo muhimu, akisisitiza kuwa lengo lao ni kufika fainali.

“Haitakuwa mechi rahisi, lakini tumefanya maandalizi mazuri. Tunaenda kupambana kupata matokeo chanya na kusonga mbele kucheza fainali,” amesema Barker.

The post KISASI CHA KIVITA NA HESHIMA AZAM NA SIMBA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/iD1QE5g
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post