NYOTA wawili wa Simba, Jean Charles Ahoua na Jonathan Sowah, wamerejea rasmi kikosini na kuungana na wenzao kambini visiwani Zanzibar, ikiwa ni maandalizi ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Ahoua na Sowah walichelewa kuingia kambini hali iliyowafanya kukosa michezo miwili ya awali ya mashindano hayo, dhidi ya Muembe Makumbi City na Fufuni SC.
Kukosekana kwao kulionekana katika baadhi ya maeneo ya kikosi, lakini benchi la ufundi liliendelea kuwapa nafasi wachezaji wengine.
Hata hivyo, kurejea kwa nyota hao wawili ni habari njema kwa Wekundu wa Msimbazi, kwani wamewahi kwa wakati muhimu kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam FC.
Simba itachuana na Azam FC katika mchezo huo utakaochezwa Januari 8, 2025, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo ushindi utaihakikishia nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo.
Benchi la ufundi linatarajiwa kuanza maandalizi maalum ya mchezo huo, likiwa na matumaini makubwa ya kunufaika na uzoefu na ubora wa Ahoua na Sowah katika pambano hilo muhimu.
The post AHOUA, SOWAH KUIWAHI NUSU FAINALI AZAM appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/uBxhIF5
via IFTTT
Post a Comment