KIUNGO kabaji wa Yanga, Mohammed Damaro amesema ujio wake ndani ya kikosi hicho umetokana na dhamira ya kupambana kwa nguvu zote ili kufikia malengo makubwa yanayotarajiwa na Wananchi msimu huu.
Damaro amejiunga na Yanga kwa mkataba wa mkopo akitokea klabu ya Singida Black Stars, ambapo atakuwa sehemu ya kikosi cha Wanajangwani kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Damaro amesema kucheza katika klabu kubwa kama Yanga ni ndoto ya kila mchezaji, hivyo kupata nafasi hiyo kunamfanya ajisikie fahari kubwa pamoja na hamasa ya ziada.
Ameongeza kuwa mazingira aliyoyakuta ndani ya Yanga yanaonesha timu iliyojipanga vizuri, jambo linalompa motisha ya kufanya kazi kwa bidii ili kuthibitisha uwezo wake ndani ya kikosi hicho.
“Nina hisia kubwa sana, kwani tangu tulipoanza safari ya kujijenga kama wachezaji, lengo lilikuwa kufika katika timu kubwa kama Yanga. Nafurahi kuwa sehemu ya familia hii ya timu nzuri,” amesema Damaro.
Damaro amesisitiza kuwa amejipanga kupambana kila anapopata nafasi ya kucheza, akitaka kutoa mchango wake kwa kiwango cha juu ili kufikia matarajio ya benchi la ufundi na mashabiki wa Yanga.
Kwa mujibu wa Damaro, Yanga ni klabu yenye malengo makubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano yote ya ndani pamoja na kufanya vizuri kimataifa, na yeye yupo tayari kuwa sehemu ya safari hiyo ya mafanikio.
The post DAMARO AJIVESHA MABOMU YANGA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/6yV9aj3
via IFTTT
Post a Comment