MENEJA wa timu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema hakuna sababu ya wapinzani kuwachukulia poa Wekundu wa Msimbazi licha ya kwenda Visiwani Zanzibar.
Amesema kikosi chenye wachezaji pungufu, timu hiyo imejipanga kuonyesha ubora wake katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Simba kwa sasa wapo Visiwani Zanzibar tayari kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo ya kihistoria, ambapo wanatarajiwa kushuka dimbani kesho Januari 3 kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Muembe Makumbi City, New Amaan Complex.
Rweyemamu amesema licha ya kikosi hicho kuwa na mchanganyiko wa wachezaji wa kikosi cha kwanza na chipukizi kutoka timu ya vijana, dhamira ya Simba imebaki ileile ya kushindana kwa nguvu zote na kupambania matokeo chanya katika kila mchezo.
Ameeleza kuwa baadhi ya wachezaji wao muhimu hawakuwepo kutokana na majukumu ya timu ya Taifa, lakini hilo halijapunguza ari ya kikosi, kwani maandalizi yamefanyika kwa umakini mkubwa kuhakikisha wanatimiza malengo yao.
“Hatujaja na kikosi kamili kwa sababu wachezaji wengi wapo kwenye timu ya Taifa, lakini tumepanga vizuri na tumekuja kuonyesha kuwa tunahitaji kulichukua kombe hili,” alisema Rweyemamu.
Meneja huyo ameongeza kuwa timu imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha inafikia malengo yake, ikiwemo kupambana kwa nidhamu, kujituma uwanjani na kulinda heshima ya klabu katika mashindano hayo.
Amesisitiza pia kuwa michuano hiyo ni fursa muhimu kwa kocha mpya wa Simba, Steve Barker, kupata nafasi ya kuliona na kulitathmini kikosi chake kwa karibu, jambo litakalompa mwanga wa kiufundi kuelekea changamoto zijazo za msimu.
The post MAZITO SIMBA ISICHUKULIWE POA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/BXjuTvG
via IFTTT
Post a Comment