AHOUA AAGANA NA SIMBA, ATUA CR BELOUIZDAD

KIUNGO  mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua, ameagana rasmi na klabu ya Simba SC baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho wake kwenda klabu ya CR Belouizdad ya nchini Algeria.

Ahoua amejiunga na miamba hiyo ya Algeria kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu, ambapo atafanya kazi chini ya kocha Sead Ramovic, aliyewahi kuinoa Yanga SC katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nyota huyo anahama Simba SC akiwa ameacha alama chanya kutokana na kiwango kizuri alichokionyesha, akionesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao pamoja na kucheza kwa nguvu katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Katika kipindi chake akiwa Simba, Ahoua alionekana kuwa mchezaji muhimu kutokana na uwezo wake wa kucheza kama mshambuliaji wa kati, pamoja na kushirikiana vyema na wachezaji wenzake katika kutengeneza na kumalizia mashambulizi.

Ubora huo ulimfanya kuwa mchezaji aliyewavutia vilabu kadhaa barani Afrika, hali iliyopelekea CR Belouizdad kuchukua hatua za haraka kunasa saini yake katika dirisha la usajili.

Kwa upande wa CR Belouizdad, usajili wa Ahoua unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kujiimarisha zaidi katika mashindano ya ligi ya Algeria pamoja na michuano ya kimataifa, wakilenga kufanya vizuri zaidi msimu huu na ijayo.

The post AHOUA AAGANA NA SIMBA, ATUA CR BELOUIZDAD appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/WNSV9E5
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post