RUSHINE, MABADILIKO BENCHI LA UFUNDI SI SAHIHI

BEKI wa Simba, Rushine De Reuck, amekiri kuwa kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids, kumeleta changamoto kwa wachezaji kadhaa, akiwemo yeye pamoja na kiungo Neo Maema, hasa kutokana na mabadiliko ya mazingira ndani ya kikosi.

De Reuck amesema kuwa hali hiyo haikuwa rahisi kwao kwani walikuwa bado wageni ndani ya timu, huku kocha aliyewaleta na kuwajengea imani akiondoka mapema.

Amessma  kuwa mabadiliko hayo yalihitaji uvumilivu na kujifunza upya namna ya kuendana na hali mpya.

Kuhusu changamoto hizo, De Reuck amesema  soka lina mambo mengi yasiyotabirika, hivyo mchezaji hana budi kukubali mabadiliko na kuendelea kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa.

Ameongeza kuwa  umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya klabu na kuendelea kupambana uwanjani.

“Mambo yalibadilika ghafla, lakini huo ndio uhalisia wa soka. Tunapaswa kuendelea kufanya kazi kwa heshima, kujituma na kuonyesha ubora wetu kila tunapopata nafasi,” amesema De Reuck.

Kwa sasa, Simba ipo chini ya kocha mpya, Steve Barker, ambaye amechukua jukumu la kukiongoza kikosi hicho kuelekea malengo yake ya msimu.

Mabadiliko hayo yamehitaji wachezaji kuzoea falsafa mpya ya ufundishaji pamoja na mbinu tofauti za mchezo.

Licha ya changamoto za mabadiliko ya benchi la ufundi, wachezaji wa Simba wamesema dhamira yao ni moja tu, kuhakikisha timu inafanya vizuri katika kila mashindano na kurejesha furaha kwa mashabiki wao.

De Reuck amesema  kuwa mshikamano ndani ya kikosi ni jambo muhimu kwa sasa, akiamini kuwa kwa kufanya kazi kwa pamoja, Simba itaweza kupita kipindi hiki cha mpito na kurejea kwenye kiwango bora kinachotarajiwa na mashabiki wake.

The post RUSHINE, MABADILIKO BENCHI LA UFUNDI SI SAHIHI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/j5HLVms
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post