SIMBA NDIO CHAGUO SAHIHI KWA MUSTAKABALI WA MORICE

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, ameweka  bayana msimamo wa klabu hiyo kuhusu hatma ya kiungo wake nyota, Abraham Morice, ambaye kwa sasa anahusishwa na tetesi za kuwindwa na wapinzani wao wa jadi, Yanga.

Magori amesema licha ya taarifa zinazosambaa kuhusu nia ya Yanga kumsajili Morice, Simba bado ipo imara na inaendelea kulinda malengo yake ya muda mrefu pamoja na wachezaji wake muhimu, kuwa hakuna sababu ya taharuki.

Akizungumza kuhusu tetesi hizo, Magori amesema viongozi wa Simba wamekuwa wakizisikia taarifa mbalimbali kuhusu mustakabali wa Morice, lakini hawajayumba wala kuvurugwa na maneno yanayoendelea kusambazwa nje ya klabu.

“Nimekuwa nikiona hizi habari za Morice kuhusishwa na Yanga, lakini ni muhimu kuweka wazi ukweli. Morice ana mustakabali mzuri sana mbele yake,” amesema Magori, akionesha imani kubwa aliyonayo kwa mchezaji huyo.

Ameongeza kuwa taarifa za aina hiyo zinaweza kumchanganya mchezaji, hasa pale zinapozidi kuenea bila msingi wa moja kwa moja, jambo ambalo linaweza kumuathiri kisaikolojia na kimchezo.

Kwa mujibu wa Magori, Simba bado ni sehemu sahihi kwa Morice kuendelea kukuza kipaji chake, kupata ushindani wa kiwango cha juu na kutimiza ndoto zake za kisoka, tofauti na kuhangaishwa na tetesi zisizo na uhakika.

Magori amesisitiza  kuwa Simba itaendelea kumlinda mchezaji wake na kuhakikisha anabaki katika mazingira bora yatakayomsaidia kufikia malengo yake, huku klabu ikiendelea kupambana kutimiza malengo yake ya ndani na kimataifa.

The post SIMBA NDIO CHAGUO SAHIHI KWA MUSTAKABALI WA MORICE appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/ifZ6y7k
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post