PAMOJA NA KUZABULIWA KIMATAIFA MARA 2….SIMBA KUNA UJUMBE WENU HAPA….

MSIMBAZI hali si shwari tangu ilipofanya Mkutano Mkuu wa mwaka Jumapili iliyopita na kisha timu hiyo kupoteza mechi ya pili mfululizo ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Stade Malien ya Mali iliyomponza Dimitar Pantev kufutwa kazi, lakini sasa wamepewa ushauri wa bure.

Pantev aliyeiongoza Simba katika mechi tano za mashindano tangu alipokabidhiwa timu kumpokea Fadlu Davids aliyerejea Raja Casablanca ya Morocco, ametangazwa kusitishiwa mkataba kwa makubaliano ya pande mbili ikiwa ni siku 61 tu tangu aanze kazi Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, katika sintofahamu iliyoanzia kwenye Mkutano mkuu uliomalizwa kiutata na Mwenyekiti, Murtaza Mangungu kabla hata marekebisho ya katiba ya klabu hiyo hayajafanyika, mastaa wa zamani wa klabu hiyo, wametoa ushauri wa kumaliza hali hiyo ili Simba isonge mbele.

Staa wa zamani wa klabu hiyo, Zamoyoni Mogella alisema: “Simba ilikuwa na projekti ya kutengeneza timu cha kujiuliza inakwama wapi, maana kila msimu inasajili wachezaji wapya na kuacha. Kwa mfumo huo projekti itakamilikaje, ndiyo maana kuna umuhimu wa viongozi kujitathimini, mpira ni wa wazi kinachofanywa na wachezaji kinaonekana.

“Japo sijafuatilia mkutano mkuu ambao pia umeacha maswali mengi sana yanayozidi kuleta jazba kwa mashabiki, Simba imefungwa mabao 2-1 na Stade Malien sababu kubwa ni kukosekana ubora wa wachezaji, mpira unahitaji unyoofu na sio ubabaifu.

“Katika usajili wa dirisha dogo ninachoweza kushauri klabu iingie gharama ya kutafuta wachezaji wenye uwezo mkubwa. Simba inaruhusu mabao ya kufungwa halafu haifungi mabao, hiyo ina maana timu nzima haipo vizuri, sasa waache kusajili wachezaji ambao hawana viwango wala hawajui malengo ya klabu.”

Mchezaji mwingine wa zamani wa timu hiyo, Emmanuel Gabriel ‘Batigol’ alisema: “Wanachama wa Simba wakubali timu inapitia vipindi vigumu, wasiishie kupiga kelele bila kuchukua hatua, kuna matawi lazima wakae namna ya kuinusuru timu kurejea katika mstari ulionyooka.

“Nimeona mechi ya Simba dhidi ya Malien hawachezi kitimu, wanapoteza mipira.”

“Ifikie hatua wanapaswa wao wenyewe kuhamasishana na kuelewa Simba ni ya ushindani na sio kubahatisha matokeo,” alisema Batigol aliyewahi kuwika pia Nazareth ya Njombe.

Steven Mapunda ‘Garrincha’ kwa upande wake alisema: “Kwanza viongozi wanapaswa kutambua wanachama wanahitaji nini kwa ajili ya kuleta maendeleo ya klabu, hivyo ni bora wakaja na tathimini nzuri ambayo italeta mwanga wa manufaa mbele, pia matawi ya Simba yakae na yenyewe yajadili kipi kitakuwa msaada kwa timu.”

The post PAMOJA NA KUZABULIWA KIMATAIFA MARA 2….SIMBA KUNA UJUMBE WENU HAPA…. appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/gZ0435S
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post