MATOLA NAFASI NDANI YA SIMBA, BARKER AMPA IMANI

KOCHA  Mkuu wa Klabu ya Simba, Steve Barker, amependekeza kocha Suleiman Matola aendelee kubaki ndani ya kikosi hicho kama kocha msaidizi namba mbili katika benchi la ufundi analotarajia kuliunda siku chache zijazo.

Barker anatarajiwa kukamilisha muundo wa benchi lake la ufundi mara baada ya kuwasili kwa kocha msaidizi namba moja, ambaye atajiunga na timu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yanayoikabili Simba katika kipindi kijacho.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Simba kimeeleza kuwa Barker anaamini uwepo wa Matola utaongeza uthabiti katika benchi la ufundi, hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa ndani ya klabu hiyo.

Imeelezwa kuwa Steve Barker na  Matola wana uhusiano mzuri wa kirafiki wa muda mrefu, hali iliyochangia kocha huyo mpya kumwona msaidizi wake huyo kama mtu sahihi wa kuendelea kufanya naye kazi.

Zaidi ya hilo, Matola anafahamika kuwa na uelewa mpana wa mazingira ya klabu pamoja na wachezaji, jambo linaloaminika litamsaidia Barker kuharakisha mchakato wa kuijenga upya Simba.

“Uzoefu wa Matola wa kukaa na wachezaji kwa muda mrefu unaelezwa kuwa faida kubwa, kwani atakuwa kiungo muhimu kati ya benchi la ufundi jipya na kikosi cha wachezaji,” amesema chanzo hicho.

Kwa mapendekezo hayo, inaonekana Simba inalenga kuunganisha uzoefu wa makocha waliopo ndani ya klabu na mbinu mpya za kocha mkuu, ili kuhakikisha timu inapata matokeo chanya na kurejesha makali yake katika mashindano yote.

The post MATOLA NAFASI NDANI YA SIMBA, BARKER AMPA IMANI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/LYdgivJ
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post