Wakati wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho wakichagua kucheza mechi zao za makundi katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, inaelezwa Simba huenda ikatumia uwanja wa Benjamin Mkapa.
Klabu za Azam Fc na Singida Black Stars ambazo zinashiriki makundi kombe la Shirikisho (CAFCC) zimethibitisha kuchagua dimba la Amaan kucheza mechi zao wakiungana na klabu ya Yanga ambayo nayo imethibitisha kuhamia Zanzibar.
Simba bado haijatoa tarifa rasmi lakini taarifa za ndani zimedokeza kuwa imewasilisha ombi lake kwa Serikali kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa ambao mapema mwezi huu Serikali ilitangaza kuufunga kutumika kwa mechi za ndani kwa kuwa bado ukarabati unaendelea.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, ilibinisha kuwa uwanja huo unaweza kutumika katika mechi za Kimataifa ingawa aliweka wazi ruhusa ya kutumika itategemea na aina ya ukarabati unaoendelea.
Simba ina rekodi ya kipekee katika michuano ya CAF ikipata matokeo mazuri kwenye mechi walizocheza dimba la Mkapa.
Mashabiki wa Simba wanaamini hakuna mpinzani mgumu mbele ya Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Vigogo wote wa soka barani Afrika walioshuka kwa Mkapa kuikabili Simba hawakutoka salama, huo umekuwa utaratibu wa kawaida kwa Mnyama.
Mechi za hatua ya makundi CAFCL zitaanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu Simba ikianzia nyumbani dhidi ya Petro Atletico
Usikose kuitazama mechi zote LIVE kupitia Simu yako pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA AU HAPAAAA au HAPAA

Post a Comment