TAARIFA MPYA KUTOKA YANGA JIONI HII


 Klabu ya Yanga imechagua dimba la New Amaan Complex kucheza mechi tatu za nyumbani hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema uamuzi wa kupeleka mechi hizo visiwani Zanzibar umezingatia maslahi mapana ya klabu baada ya kufanyika tathmini ya kina.

"Baada ya uongozi kufanya Tathimini na kuangalia maslahi mapana ya klabu yetu, nipende kuwatangazia kuwa mechi zetu zote 3 za nyumbani kwenye hatua ya Makundi, tutatumia uwanja wa New Amaan Comolex, Zanzibar."

"Niwaombe sana mashabiki na Wanachama wetu kutoka visiwa vya Pemba na Unguja kujiandaa kuipokea timu na maandalizi ya nguvu kuelekea mchezo wa kwanza wa nyumbani dhidi ya FAR RABAT."

"Wanachama wengine kutoka mikoani tujiandae pia, tupo kwenye kundi gumu lakini tukiwa wamoja, tukiendelea kushiriana kwa umoja wetu tutatoboa, " alisema Kamwe.

Usikose kuitazama mechi zote LIVE kupitia Simu yako pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA  AU HAPAAAA au HAPAA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post