Yanga kujipima dhidi ya Jkt tanzania Kesho


 Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amehitaji mechi zaidi za kirafiki kabla ya kikosi chake kutambulishwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya wiki tatu za mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili, kwa sasa Folz amejikita zaidi katika maandalizi ya kimbinu na ili kufanya tathmini ya kiasi gani wachezaji wake wameiva, ni kupitia mechi hizo za kirafiki

Mpaka sasa Yanga imecheza mechi nne za kirafiki katika kipindi hiki cha pre-season moja ikiwa ya ndani dhidi ya Yanga U20

Mechi nyingine tatu ilikuwa dhidi ya Rayon Sport, Fountain Gate na Tabora United ambazo zote Yanga ilishinda

Kesho Yanga inatarajiwa kujipima dhidi ya JKT Tanzania katika mwendelezo wa mechi hizo za kunoa silaha

Katika kilele cha wiki ya Mwananchi Yanga itaumana na Bandari Fc ya Kenya siku nne kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 16

Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope ukisha download App utaweza kuona chanel hivi👇🏻👇🏻

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post