Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, ameweka bayana imani yake kubwa kwa kiungo mpya wa timu hiyo, Mohamed Doumbia, akimtaja kama miongoni mwa wachezaji watakaobeba timu hiyo msimu ujao.
Doumbia, aliyesajiliwa kwenye dirisha hili la usajili, amekuwa kivutio kikuu katika kambi ya maandalizi ya Yanga inayoendelea Avic Town, huku kila aliyejionea uwezo wake akionekana kushawishika kwamba klabu hiyo imepata “nyota wa kipekee.”
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika Mwananchi Day itakayofanyika Septemba 12 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ili kujionea wenyewe kipaji cha Doumbia.
“Huyu mtu ni hatari sana ndugu zangu, Septemba 12 njooni kwa wingi mthibitishe kile ninachosema. Hivi vitu anavyofanya hapa Avic Town na mechi za kirafiki ni hatari, sema tu kwa sababu hatuzionyeshi. Lakini mimi muda wote nipo Avic Town nawaambia tumepata mchezaji wa daraja la juu,” alisema Kamwe.
Kwa mujibu wa Kamwe, Doumbia ana uwezo unamuweka katika daraja moja na nyota wengine mahiri katika kikosi cha Yanga akiwemo Pacome Zouzoua.
“Doumbia unaweza kumuweka daraja moja na kina Pacome, mambo anayofanya ni ya viwango vya hali ya juu. Wakati wengine wanaolalamika kutokuwa na wachezaji wa kuwatisha wapinzani, sisi huku tuna Doumbia na wengine wengi,” aliongeza.
Doumbia tayari ameonekana kuwa gumzo kubwa kambini, akitajwa na wachezaji wenzake na benchi la ufundi kama nyota mwenye akili ya mpira na uwezo wa kipekee.
Ni wazi, mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu siku ya Mwananchi ili kushuhudia..
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au Bonyeza HApa Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope ukisha download App utaweza kuona chanel hivi👇🏻👇🏻
.jpeg)
Post a Comment