Baada ya mapumziko ya siku takriban tatu kikosi cha Simba jana kimerejea kambini kujiandaa na Tamasha la Simba Day, lakini kubwa zaidi ni kuiwinda Yanga, katika mchezo wa Ngao ya Jamii, unaotarajiwa kuchezwa, Septemba 16, mwaka huu na mechi za ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inasema kuwa baada ya kuingia kambini jana, kikosi hicho hakitakuwa na mapumziko yoyote hadi kitakapocheza mchezaji wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, Septemba 20, mwaka huu, nchini Botswana.
"Tulipowasili tu kocha Fadlu David,s alitoa mapumziko kwa wachezaji kwani walikuwa wametumika kwa wiki nne wakifanya mazoezi magumu"
“Aliwaachia wakaenda kusalimia familia zao, leo (jana) tunaingia tena kambini, mazoezi kama kawaida tupo Mo Arena Bunju, hapa tena hakuna mapumziko mpaka tucheze michezo mitatu muhimu inayotukabili mbele yetu," alisema mtoa taarifa ndani ya klabu hiyo.
Simba itacheza dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Septemba 10 kwenye kilele cha Simba Day, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambapo mbali na burudani, wanachama watapata fursa ya kukifahamu kikosi chao cha msimu wa 2025/26, wakiwamo wachezaji wapya.
Simba itacheza dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Septemba 10 kwenye kilele cha Simba Day, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambapo mbali na burudani, wanachama watapata fursa ya kukifahamu kikosi chao cha msimu wa 2025/26, wakiwamo wachezaji wapya.
Baada ya hapo kikosi hicho kitasafiri kwenda nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United utakaochezwa, Septemba 20, kabla ya marudiano Septemba 26, mwaka huu, hapa nchini.
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.
.jpeg)
Post a Comment