Nangu , Yacoub wasubiriwa Msimbazi


 Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema anawasubiri nyota wapya beki Wilson Nangu na mlinda lango Yacoub Suleiman kambini waungane na timu ili ajue namna ya kuwatumia, licha ya kujua uwezo waliouonyesha wakiwa JKT Tanzania na hata Stars.

Simba imemalizana na nyota hao wawili waliokuwa Stars iliyoshiriki fainali za CHAN 2024 zilizoandaliwa kwa ushirikiano wa nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda ikiwang’oa kutoka JKT Tanzania iliyowapa ‘thank you’ wiki iliyopita kuonyesha kuwa hawakuwa na maafande hao.

Hata hivyo, juzi kocha Fadlu anayejiandaa kuiongoza kwa msimu wa pili mfululizo katika michuano ya msimu huu wa 2025-2026, amevunja ukimya na kusema anatambua viwango vya juu walivyoonyesha wachezaji hao wapya wakiwa na JKT msimu uliyopita, kitu kinachomwaminisha watafanya vizuri Ligi Kuu inayoanza Septemba 17.

Nangu alimaliza na mabao mawili na asisti mbili, Yakoub akiwa na clean sheets nane, kila mmoja amesaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo ya Msimbazi, lakini walikuwa bado hawajajiunga kambini kutokana na jukumu ya timu ya taifa inayojiandaa na mechi za kuwania Fainali za Kombe la Dunia za 2026 ikitarajiwa kucheza mechi mbili - Septemba 5 na 9.

Kutokana na hilo, kocha Fadlu alisema anawasubiri kuwaona kambini aungane nao, pamoja na kutambua uwezo walionao na awaliouonyesha wakiwa JKT Tanzania na hata Taifa Stars.

“Pamoja na hayo yote ninaamini ni vijana ambao wanajua kipi wanakitafuta katika mpira wa miguu, kwa namna ambavyo walikuwa wanapambana kuhakikisha wanaisaidia timu ya JKT Tanzania kufanya,” alisema Fadlu

“Ni wachezaji wazuri kwa kile nilichokiona wamekifanya katika ligi msimu uliyopita, kila mmoja kwa nafasi yake kipa ana umakini wa kuokoa hatari na beki anajitoa na anatumia nguvu,” alisema Fadlu.

“Kuhisiana na wataongeza kitu gani kikosini, kwa sasa siwezi kulizungumzia hilo kwa sababu bado hawajaingia kambini, ningewaona katika mazoezi na wenzao ningekuwa na kitu kikubwa cha kuwaelezea.

Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post