Yanga watambulisha kitu kipya kuelekea Siku ya Mwananchi

 


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa 'level' ambayo Yanga imefikia sasa haihitaji tena kaulimbiu za kupeana matumaini

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Kamwe alitangaza kaulimbiu ya Yanga kuelekea Wiki ya Mwananchi, kaulimbiu ambayo Wananchi wataitumia msimu mzima

TUNAPIGA KICHWANI TU ndio kaulimbiu maalum kuelekea Wiki ya Mwananchi, Kamwe akifafanua kuwa kaulimbiu hiyo inamaanisha kila atakayekuja mbele ya Yanga atakumbana na kipigo kizito

"Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini, tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi"

"Kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu. Hiyo ndio slogan yetu, Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwani tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu"

"Kama umesajili wachezaji wako waliopewa mkono wa kwaheri huko walikotoka basi ujue watakutana na nyundo. Kuna nyundo ya Boyeli tena yeye anapenda kupiga kwenye vpara"

"Tuna nyundo za akina Bacca hapigi tena kwenye ugoko, anapiga kichwani tu. Kama mmefanya sajili za kuunga unga basi tunaenda kupiga mafuvu sugu," alitamba Kamwe

Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post