SIMBA KUJA KIVINGINE MECHI YA KESHO DHIDI YA YANGA


 Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga akisema kuwa kikosi chake kitakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji tofauti na walivyocheza mechi dhidi ya Gor Mahia

Baada ya kuhitimisha Tamasha la Simba Day kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia, Simba ilirejea kambini kujiwinda na mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho, Jumanne kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Fadlu amekiri kuwa mchezo hautakuwa mwepesi kwani ni mchezo wa dabi ambao wanakutana na mpinzani ambaye yuko imara pia

“Tunaendelea kujipanga na mchezo wa Ngao ya Jamii, ninaamini tutakuwa sawa, tunafanya maandalizi sahihi kuelekea mchezo huo”

“Najua kiu ya Wanasimba wengi ni kuona tunafanya vyema katika mchezo huo na michuano yote ambayo iko mbele yetu ili kutimiza malengo ya klabu"

 “Simba ni timu kubwa, baada ya kazi kubwa ya kujenga timu tuliyofanya msimu uliopita, naamini msimu huu tuko tayari kushindana,” alisema Fadlu

Itakuwa mechi ya nne kwa Fadlu kukabiliana na Yanga akiwa amepoteza mechi tatu zilizopita. Hivyo mechi ya kesho itakuwa na umuhimu wa kipekee kwake na benchi la ufundi

Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post