Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeifungia klabu ya Simba kucheza bila ya mashabiki mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United, mchezo utakaopigwa Septemba 27 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, imefahamika
Kulingana na taarifa ya CAF, adhabu hiyo imetokana na matukio ya vurugu yaliyojitokeza katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry msimu uliopita
Aidha baada ya kutumikia adhabu hiyo, Simba itaendelea kuwa katika uangalizi na endapo matukio ya vurugu yatajitokeza tena huenda ikakumbana na adhabu kubwa zaidi
Hii ni habari mbaya kwa mashabiki wa Simba ambao sasa watalazimika kuishuhudia timu yao pale dimba la Mkapa kupitia televisheni ikichuana na Gaborone United
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au Bonyeza HApa Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment